1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antony Blinken amekutana na Volodymyr Zelensky mjini Kiev

14 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana leo na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kiev akiwa katika ziara yake ya kidiplomasia ambayo haikutangazwa.

https://p.dw.com/p/4fqD0
Ukraine | Antony Blinken na Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukrainia Volodymyr Zelenskyy, kushoto, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kulia, kabla ya mkutano wao mjini Kyiv, Ukraine, Jumanne, Mei 14, 2024.Picha: Ukrainian Presidential Press Office/AP/picture alliance

Ziara hiyo ya siku mbili inalenga kuihakikishia Ukraine kwamba Marekani inaiunnga mkono wakati ikipambana kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi yaliyoongezeka. Aidha ziara hiyo imekuja chini ya mwezi mmoja,baada ya bunge la Marekani kuidhinisha msaada wa dola bilioni 60 kwa Ukraine,fedha ambazo zitaisadia nchi hiyo kuongezasilaha na mifumo yake ya ulinzi. Aidha Ukraine hivi sasa inapambana kuwahamisha raia wake kutoka mji wa Vovchansk katika mkoa wa Kharkiv ambako Urusi inasogelea.Ni ziara ya nne ya Blinken mjini Kiev tangu Urusi kuivamia Ukraine Februari mwaka 2022.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW