1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa 'uchokozi wa kijeshi'

7 Septemba 2023

Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa kuandaa uchokozi wa kijeshi dhidi ya vikosi vyake, kwa kuweka wanajeshi kwenye mpaka wa pamoja karibu na eneo lililojitenga la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4W4pW
Armenien - Bergkarabach Konflikt
Picha: Artem Mikryukov/REUTERS

Mvutano kati ya Baku na Yerevan umeongezeka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni, huku pande zote mbili zikishutumiana kwa mashambulizi ya mpakani.

Soma pia: EU kuujadili mgogoro wa Azerbaijan na Armenia

Akizungumza katika mkutano na baraza la mawaziri huko Yerevan, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, amesema hali ya kijeshi na kisiasa katika eneo lake imezidi kuwa mbaya.

Azerbaijan imekanusha madai ya kuhusika na uchokozi wa kijeshi kwa kusema kwamba huo ni "udanganyifu wa kisiasa."

Madai ya Pashinyan yanajiri kabla ya uchaguzi wa mapema wa rais katika eneo linalotaka kujitenga la siku ya Jumamosi na siku chache kabla ya mazoezi ya pamoja kati ya vikosi vya kulinda amani vya Armenia na Marekani vilivyoandaliwa na Yerevan.