1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Armenia yasema watu 85,000 wamekimbia Nagorno-Karabakh

29 Septemba 2023

Serikali ya Armenia imesema watu wapatao 88,780 wameomba hifadhi nchini humo, baada ya Azerbaijan kuchukua udhibiti wa eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4Wx21
Watu wakiondoka Nagorno Karabakh
Msururu wa magari ya watu wanaolikimbia jimbo la Nagorno Karabakh na kuingia Armenia Picha: DAVID GHAHRAMANYAN/REUTERS

Msemaji wa serikali ya Yerevan Nazeli Baghdasaryan, amesema hii leo kuwa watu hao wamelazimishwa kuondoka nyumbani mwao.

Taarifa zimeeleza kuwa zaidi ya nusu ya wakaazi wa Nagorno-Karabakh wanaokadiriwa kufikia 120,000 tayari wamelikimbia jimbo hilo wakihofia kushambuliwa kutoka upande wa Azerbaijan.

Mamlaka za Azerbaijan zimekuwa zikiahidi kuheshimu haki za watu wa jamii ya Armenia katika eneo hilo.

Kuna hatari ya mzozo huo uliodumu kwa miongo mitatu kuwa na mwelekeo wa kidini hasa ikizingatiwa kuwa Waarmenia ni Wakristo wa madhehebu ya Orthodox, wakati idadi kubwa ya raia wa Azerbaijan ni Waislamu.