ASEAN; Myanmar haipaswi kufikiria uchaguzi kwa sasa
19 Januari 2025Wakati kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoongezeka, haupaswi kuwa kipaumbele,na kuitaka serikali hiyo kuanzisha mazungumzo ya kumaliza uhasama mara moja.
Soma pia:ASEAN yatiwa wasiwasi na mapigano Myanmar
Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Mohamad Hasan, amesema Jumuiya hiyo imetoa wito kwa pande zinazopigana nchini Myanmar kusitisha mapigano na kushauri mwakilishi wa jeshi kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kiutu iliyozuiliwa.
Malaysia kama nchi inayochukua uenyekiti wa jumuiya ya ASEANmwaka huu, imesema inataka kujua mustakbali wa Myanmar.
Myanmar imekuwa katika machafuko tangu mapema 2021 wakati jeshi lilipindua serikali ya kiraia iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi, na kusababisha maandamano ya kuunga mkono demokrasia ambayo yaligeuka kuwa uasi wa silaha.