1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASHGABAT: Rekodi ya haki za binaadamu yashutumiwa

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwb

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir hapo jana ameshutumu rekodi ya haki za binaadamu ya Turkmenistan wakati wa ziara yake nchini humo.

Jimbo hilo la zamani la Muungano wa Urusi limekuwa likishutumiwa kwa kuwakandamiza wapinzani wa utawala wake. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amewaambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na Rais Saparmurat Nijasov katika mji mkuu wa Ashgabat kwamba pia amezungumzia suala la kuzorota kwa mageuzi ya kidemokrasia nchini humo.

Ziara ya Steinmeir katika eneo hilo inakusudia kuangalia njia za kuboresha ushirikiano kati ya mataifa ya Asia ya Kati na Umoja wa Ulaya.