1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Asif Ali Zardari achaguliwa kuwa rais mpya wa Pakistan

9 Machi 2024

Wabunge nchini Pakistan, leo wamemchagua Asif Ali Zardari kuwa Rais wa nchi hiyo kwa mara ya pili.

https://p.dw.com/p/4dL10
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari Picha: AP

Zardari alipata kura 411 kutoka kwa wabunge wa bunge la taifa na mabaraza ya wawakilishi ya majimbo huku mpinzani wake, Mehmood Khan Achakzai, anayeungwa mkono na chama cha waziri mkuu wa zamani aliye gerezani Imran Khanakipata kura 181

Waziri mkuu wa Pakistan ampongeza Zardari

Waziri mkuu wa nchi hiyo Shehbaz Sharif amempongeza Zardari kwa ushindi huo.

Katika taarifa, Shariff amesema kuwa Zardari atakuwa ishara ya uthabiti wa taifa hilo.

Soma pia:Wabunge wa Pakistan wamchagua Shehbaz kuwa waziri mkuu

Mpinzani wa Zardari, Mehmood Khan Achakzai Achakzai pia amempongeza mwanasiasa huyo kwa ushindi huo na kusema kura hiyo ilifanyika kwa njia huru na haki.