1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Askari 15 wa Chad wauawa katika operesheni ya Boko Haram

11 Novemba 2024

Msemaji wa jeshi nchini Chad, Jenerali Issakh Acheikh, amesema takriban wanajeshi 15 wa nchi hiyo wameuawa na wengine 32 wamejeruhiwa katika operesheni ya jeshi dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram.

https://p.dw.com/p/4mrux
Wanajeshi wa Chad
Chad ni mshirika muhimu kwa vikosi vya Ufaransa na Marekani katika kupambana na uasi Afrika MagharibiPicha: Steven Lewis/Zuma/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Chad ameongeza kusema wapiganaji 96 wa Boko Haram pia waliuawana wengine 11 walijeruhiwa kwenye operesheni hiyo ya siku ya Jumamosi na kwamba silaha na vifaa vingine vya wapiganani wa Boko Haram vimekamatwa.

Soma pia: Wanajeshi wa Chad wauwawa katika mapambano na Boko Haram

Kwa miaka 12 sasa Chad ni mshirika muhimu kwa vikosi vya Ufaransa na Marekani katika kupambana na uasi unaoendeshwa na wapiganaji wenye misimamo mikali katika nchi za Afrika Magharibi kwenye eneo Sahel. Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na waasi wakiwemo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu katika Afrika Magharibi na kundi la Boko Haram. Mashambulizi hayo yalianzia kaskazini mashariki mwa Nigeria mnamo mwanmo mwaka 2009 na kuenea hadi magharibi mwa Chad.