Askari 2 wa AU wauliwa Dafir
20 Agosti 2006Matangazo
DAFUR/SUDAN:
Umoja wa nchi za kiafrika umearifu kwamba wanajeshi wake wawili wameuliwa na weengine 3 wamejeruhiwa baada ya mlolongo wao kuviziwa na kushambuliwa huko Dafur,Sudan.Machafuko huko Dafur yameongezeka licha ya kutiwa saini kwa mapatano ya amani yaliosimamiwa na UA hapo Mei kati ya serikali ya Khartoum na waasi.Hujuma hjiyo imetokea katika eneo linalodhibitiwa na waasi ambao hawakutia saini mapatano hayo.