1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assad atapata ujumbe ? Waulize Warusi na Iran

Sekione Kitojo
15 Aprili 2018

Maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani hawana hakika iwapo mashambulizi dhidi ya Syria yatafanikisha lengo la kuzuwia utawala wa Assad kutumia tena silaha za sumu. Lakini mashambulizi hayo yamepeleka ujumbe muhimu wa ziada.

https://p.dw.com/p/2w4B0
Zypern Britischer Kampfjet vor Einsatz
Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Matthews

Utawala  wa  Trump  uliweka  wazi kwamba  mashambulizi dhidi  ya mpango wa  silaha  za  sumu  wa  Syria  yalikuwa  na  lengo  moja: Kumzuwia rais  wa  Syria Bashar al-Assad  kutumia  silaha  kama hizo  tena hapo  baadaye kama  alivyofanya, Marekani  na  mataifa mengine  yamesema, hivi karibuni  katika  mji  wa  Douma.

Syrien Krieg - Damaskus nach Angriff durch die USA, Frankreich & Großbritannien | Scientific Research Centre
Mabaki ya nyumba baada ya shambulizi la mataifa matatu washirika nchini SyriaPicha: Reuters/O. Sanadiki

Mashambulio ya siku  ya  Ijumaa usiku yalikuja mwaka mmoja  baada ya  Marekani  kushambulia utawala  wa  Assad  kwa  namna  hiyo baada  ya Syria kudaiwa  kufanya  shambulio  baya  la   gesi  ya sumu  katika  mji  wa  khan Sheikhoun. Mara  hii , hata  hivyo, Marekani  haikuchukua  hatua  peke  yake, na yenyewe  pamoja  na Ufaransa  na  Uingereza, zilifanya mashambulizi mengi  zaidi  kuliko mwaka  mmoja  uliopita.

Hatua  hiyo  iliyoongozwa  na Marekani , iliyoelezwa  kama shambulio  moja  kubwa, lilikuwa  kilele  cha  hatua zenye vurumai kubwa  kuelekea  hatua  za  kuingilia  kati  ambazo  zilianzia, kama ilivyokuwa  kawaida  kwa  Marekani , kwa rais kuandika  katika ukurasa  wa  Twitter. Katika  ujumbe  huo, Trump  aliahidi  hatua  za haraka  na  kali  za  kijeshi , akimshutumu Assad na  kuzikejeli Urusi na  Iran. Maandishi  hayo  ya  Twitter yalizusha tahadhari  kimataifa juu  ya shambulio  ambalo litatokea katika  moja  kati  ya  maoneo yenye  matatizo  na kuwaacha  maafisa wa Marekani  wakijaribu kutafuta  majibu.

Wakati  shambulio  hilo  lilipotokea , siku kadhaa baada  ya  Trump kutoa muda  wa  awali, kulikuwa na  washirika  wawili  na mtazamo wa kupunguza malengo  ya  mashambulizi  hayo. Kwa  wachunguzi wengi , hatua  hizo  za  kijeshi  zilionekana  zaidi  kama  jibu lililowekewa  mipaka  zaidi  kuliko shambulio  kubwa  ambalo lilielezwa  hapo  kabla  na Trump. Hali  hiyo  imesababisha  maswali kadhaa.

London Pressekonferenz Theresa May zur Militäraktion in Syrien
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May Picha: Getty Images/S. Dawson

Je Assad atapata  ujumbe  na  kujizuwia  kutumia  silaha  za  sumu ?

"Sina  shauku," amesema Ryan Crocker , balozi  wa  zamani  wa Marekani  nchini  Syria, ambae  pia  alifanyakazi  kama  mjumbe  wa Marekani  nchini  Iraq, Afghanistan  na  Pakistan. "Tulifanya  kitu kama  hicho mwaka  mmoja  uliopita  katika  kiwango  kidogo. lakini mashambulizi  haya hayatafanya  uharibifu  wa  kudumu  kwa  uwezo wa  Assad wa  kutumia  silaha  za  sumu hapo  baadaye  ama kitu kingine zaidi.

"Hilo ni swali  ambalo  linabaki wazi,"  amesema  Philip Breedlove, kamanda wa  zamani  wa  NATO  na  jeshi  la  Marekani  barani Ulaya. "Kumbuka  kwamba mhalifu  huyu, kiongozi   huyu  zimwi  wa Syria , anapata  uungwaji  mkono  na  uwezo  na uungwaji  mkono wa  kisiasa  kutoka  Urusi  na Iran."

Wakati  ni  vigumu  kutabiri  jibu  la  Assad, kubadili utaratibu  wake utahitaji  hatua  ambazo  zinatishia  msingi  halisi wa  utawala  wake, amesema Mona Yacoubian , msomi  raia  wa  Syria  katika  taasisi ya  amani  ya  Marekani. Katika  hali  hiyo , mashambulizi  haya huenda ni madogo  sana  kutimiza  lengo.

USA - Trump ordnet Militärschlag auf Syrien an
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Wataalamu  wote  watatu  wamezungumzia  ushawishi  wa  Urusi  na Iran katika  utawala  wa  Assad. "Kumbuka  kwamba  Bwana  Assad binafsi  hana  uwezo wa  mambo  yote  haya  ambayo  yanatokea karibu  yake,"  amesema  Breedlove. "Anapata  uwezo, anapewa nguvu  na  kuhimizwa  na  Urusi  na  Iran."

Kwa upande  wake  viongozi  wa  mataifa  ya  kiarabu , akikosekana rais Bashar al-Assad  wa  Syria  wamekutana  nchini  Saudi Arabia kwa  ajili  ya  mkutano  unaofanyika  leo  wakati mataifa  yenye nguvu  dunaini yakipambana  kuhusu  Syria  na  hali  ya  wasi  wasi ikiongezeka kati  ya  Riyadh  na  Tehran.

Saudi Arabia  inataka  kupatikana  msimamo  mkali , na  wa  pamoja dhidi  ya  hasimu  yake  mkubwa  Iran  katika  mkutano  huo  wa  kila mwaka  wa  mataifa  22  wanachama  wa Jumuiya  ya  mataifa  ya Kiarabu, Arab league.

Ägypten Minister der Arabischen Liga tagen in Kairo | Generalsekretär Ahmed Aboul Gheit
Katibu mkuu wa Arab League Ahmed Aboul GheitPicha: Reuters/M. Abd El Ghany

Mataifa  hayo  makubwa katika  eneo  la  mashariki  ya  kati, yanapigana  vita  nchini  Syria, na katika  eneo  la  kusini  mwa Saudi  Arabia  katika  nchi  jirani  ya  Yemen, yakiunga  mkono pande  zinazopingana  nchini  Iraq  na  Lebanon.

Mwandishi:   Sekione  Kitojo / afpe

Mahariri: John Juma