1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Assad wa Syria kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Kiarabu

19 Mei 2023

Viongozi wa mataifa ya Kiarabu wanatarajiwa kumkaribisha tena rais wa Syria Bashar al Assad katika mkutano wao wa kilele nchini Saudi Arabia unaotarajiwa kujadili mgogoro wa Sudan na Yemen.

https://p.dw.com/p/4RZLF
Rais wa Syria Bashar al-Assad (mwenye suti nyeusi) akilakiwa mjini Jeddah, Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Rais wa Syria Bashar al-Assad (mwenye suti nyeusi) akilakiwa mjini Jeddah, Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.Picha: SPA/AFP

Assad aliwasili jana mjini Jeddah kwa mkutano huo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, huu ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipopigwa marufuku ya kutoshiriki mwaka 2011, kufuatia kamata kamata aliyoifanya kwa waandamanji waliokuwa wanadai demokrasia nchini Syria, iliyosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad, amesema mkutano huu ni muhimu kwa Syria na wamekuja kuufanikisha. Hata hivyo, Qatar imesema haitojaribu kuwa na mahusiano ya kawaida na serikali ya Assad.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Khaled Manzlawiy amesema mkutano huo utazungumzia pia vita vya Ukraine na mgogoro wa kiuchumi unaoukumba dunia kwa sasa.