SiasaNiger
AU yazungumzia hali ya afya ya rais aliyepinduliwa Niger
11 Agosti 2023Matangazo
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema vitendo vinavyodaiwa kufanywa na viongozi wa mapinduzi dhidi ya Bazzoum havikubaliki.
Mkuu wa shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres pia wamezungumzia kuhusu hali mbaya aliyonayo Bazoum na familia yake.
Wakati huo huo, wakuu wa kijeshi wa Jumuia ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS watakutana wiki ijayo kuuzungumzia mzozo wa Niger.
Duru za kijeshi zimeeleza leo kuwa maafisa hao wa kijeshi watakutana Ghana kuandaa mipango ya uwezekano wa kuivamia Niger kijeshi.