Aung San Suu Kyi ajitetea Mahkamani
27 Mei 2009Mkereketwa wa demokrasia wa Myanmar, Bibi Aug San Suu Kyi, ametaja ukosefu wa ulinzi wa kutosha upande wa utawala wa kijeshi wa Myanmar kuwa ndio sababu ya muamerika John Yettaw, kuogolea hadi nyumbani mwake-hii ni kwa muujibu wa taarifa yake iliotolewa leo Mahkamani.
Mshindi huyo wa Zawadi ya amani ya Nobel, alisema katika taarifa iliochapishwa na chama chake kuwa hawezi kutwikwa jukumu la kujiingiza Mmarekani huyo nyumbani mwake na kwamba, yeye hana hatia yoyote katika mashtaka aliofunguliwa kuwa alikiuka masharti ya kizuizi chake.
Bibi Aung San Suu Kyi, katika taarifa yake amejitetea kwamba hakuripoti haraka mkasa wa kujiingiza Muamerika huyo nyumbani mwake kwa utawala wa kijeshi ili kutowaponza maafisa wa usalama au muamerika Yettaw.
Lakini alisema sababu kuu ya kisa hiki ni ukosefu wa usalama wa kutosha au kutokuwapo kabisa kwa ulinzi.Akadai hakuna hatua iliochukuliwa kwa uzembe wa walinzi bali ni yeye tu aliechukuliwa hatua ya kufunguliwa mashtaka.
Taarifa ya Bibi Suu Kyi, ni yenye maelezo zaidi kuliko ile fupi aliotoa maswali wakati akihojiwa na Mahakimu alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwsanza kwenye gereza la Yangon jana alipokanusha hatia yoyote upande wake.
Taarifa yake ilisema kwamba alitoa taarifa kwa maafisa wa serikali kwa mara ya kwanza hapo nov. 2008 lakini wakati ule hawakuchukua hatua yoyote na wsala hawakumuonya kuripoti visa vyovyote vile vinavyoweza kutokea baadae.
Yettaw, alimtembelea kwa mara nyengine Mei 4,mwaka huu-alisema.Alim,uomba kuondoka ,lakini alimjibu aweza kukamatwa kwavile usubuihi ilikwishaingia .Alimuahidi angeondfoka usiku.Ulipoingia usiku aliomba abaki kwavile, afya yake haikuwa nzuri.
Mshindi huyu wa Tuzo la Amani la Nobel ,mwenye umri wa miaka 63 aliarifu kuwa baada ya Mumareika John Yettaw kuondoka nyumbani mwake, alipanga kumuarifu daktari wake alipomtembelea hapo Mei 7 ili nae aiarifu serikali.Lakini, daktari huyo alizuwiliwa kumuona. Akasema kwamba,pale polisi walipomjia siku hiyo,baada ya kumkamata Muamerika Yettaw hapo Mei 6,walionesha wameridhia nilivyofanya kwavile ,hawakuonesha upinzani wowote au kukosoa kwa aina yoyote ile.
Bibi Aung San Suu Kyi ,alikanusha pia dai lililotolewa na afisa wa polisi alietoa ushahidi mahkamani kuwa binafsi alikuwa na jukumu la usalama nyumbani mwake.
Amri ya kumweka kizuizini nyumbani tangu Mei ,2003 binafsi ni kinyume na sheria,kwavile amri hiyo imo ndani ya katiba ambayo imevunjwa na utawala binafsi wa kijeshi wa Myanmar.
Bibi Aung San Suu Kyi, anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 5 korokoroni,endapo akikutikana na hatia.
Rais Barack Obama wa Marekani jana aliwataka majamadari wanaotawala Myanmar kumuacha huru kiongozi huyo wa Upinzani tena haraka na bila ya masharti yoyote.
Obama lierefusha vikwazo vya Marekani kwa utawala wa M yanmar hapo mei 15, alieleza kuwa mashtaka dhidi ya Bibi Suu Kyi yanaleta shaka kuwa serikali ya Myanmar itayari kweli kuchukluliwa ni mmwanachama mwenye dhamana wa jamii ya kimataifa.
Muadishi: Ramadhan Ali/AFPE
Mhariri:M.Abdul-Rahm