AfyaAustralia
Australia: Mama mmoja atolewa mnyoo hai kwenye ubongo wake
29 Agosti 2023Matangazo
Mnyoo huo alikuwa na urefu wa sentimeta 8.
Aina ya mnyoo huo kwa jina Ophidascaris robertsi unapatikana zaidi kwenye baadhi ya chatu na kwa kawaida huingia katika miili ya viumbe wengine lakini si miili ya binadamu.
Wanasayansi nchini Australia wamechapisha taarifa juu ya mkasa huo usiokuwa na kifani.
Mwanamke aliyetolewa mnyoo huo alikuwa analalamika kusumbuliwa na maumivu kwa muda mrefu.