Awamu ya 6 ya Karandinga kwa njia ya kidijitali!
Karandinga imebadilika na sasa inakuletea muundo mpya wa simulizi za hadithi! Katikati ya vizuizi vilivyowekwa kuzuia kusambaa kwa COVID-19, kwa msaada wa vifaa vya kisasa vya kidijitali, michezo yetu bado inaendelea.
Karandinga inakuletea muundo mpya
Grace Patricia Kabogo (Kushoto), mtayarishaji na mwandaaji wa vipindi vya Karandinga akiwa Bonn-Ujerumani, Michael Springer (Kulia), Fundi Mitambo akiwa Cologne-Ujerumani pamoja na Editha Mayemba (Katikati), Muigizaji akiwa Dar es Salaam, Tanzania wakitumia vifaa vya kisasa vya kidijitali kurekodi mchezo mpya wa Karandinga, katikati ya vizuizi vilivyowekwa kuzuia kusambaa kwa janga la COVID-19.
Simulizi kwa njia ya kidijitali
Editha Mayemba muigizaji wa michezo ya Karandinga, akisimulia moja ya hadithi mpya za michezo ya Karandinga zilizorekodiwa kwa mfumo wa kidijitali, akiwa katika studio zetu zilizoko jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Siku imekamilika
Timu ya Karandinga: Grace Patricia Kabogo (Kushoto), mtayarishaji na mwandaaji wa vipindi vya Karandinga, Michael Springer (Kulia), Fundi Mitambo pamoja na Editha Mayemba, muigizaji na Simon John mtayarishaji msaidizi, waliofanikisha kurekodiwa mchezo mpya wa ''Karandinga'', kwa kutumia vifaa vya kisasa vya kidijitali, katikati ya vizuizi vilivyowekwa kuzuia kusambaa kwa janga la COVID-19.
Umakini wakati wa kurekodi
Michael Springer, Fundi Mitambo wa vipindi vya Karandinga akiwa mjini Cologne-Ujerumani, akifuatilia kwa umakini jinsi vifaa vya kisasa vya kidijitali vinavyorekodi michezo ya Karandinga kwa kutumia mfumo wa simulizi ya hadithi.
Matayarisho kabla ya kurekodi
Kama ilivyo kawaida kabla ya kurekodi michezo ya Karandinga huwa tunawapa muda waigizaji muda wa kufanya mazoezi. Pichani muigizaji Editha Mayemba akipitia moja ya hadithi alizorekodi kwa njia ya kidijitali.
Mfumo wa kidijitali
Vifaa vya kisasa vya kidijitali vimefanikisha kurekodi michezo ya Karandinga ya awamu ya 6 katikati ya vizuizi vilivyowekwa kuzuia kusambaa kwa janga la virusi vya corona, tumeendelea kuandaa michezo yetu barani Afrika – kwa mbali!