SiasaAzerbaijan
Azerbaijan, Armenia mbioni kufikia makubaliano ya amani
23 Aprili 2024Matangazo
Timu kutoka nchi hizo mbili zitaweka alama kwenye mpaka kulingana na ramani za enzi ya Kisovieti. Rais Aliyev ameongeza kuwa.
"Hatukuwa na rasimu ya makubaliano ya amani wakati huo, lakini sasa tunayo. Sasa tuna uelewa wa pamoja wa jinsi makubaliano ya amani yanapaswa kuwa. Tunahitaji tu kushughulikia maelezo".
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mwezi uliopita alikubali ombi la Azerbaijan la kurudisha vijiji vinne vya mpaka ambavyo vilikuwa sehemu ya Azerbaijan wakati nchi hizo mbili zilipokuwa Jamhuri za Muungano wa Kisovieti.