Azerbaijan na Armenia kuzungumza kuhusu Nagorno Karabakh
26 Septemba 2023Matangazo
Maafisa wa Nagorno Karabakh pia wamearifu kwamba watu wasiopungua 20 wameuwawa na wengine takriban 300 wamejeruhiwa kufuatia mripuko uliotokea katika kituo cha kujaza gesi wakati watu wakihangaika kukimbilia Armenia.
Soma pia:Maelfu wahama Nagorno-Karabakh kukimbilia Armenia
Mkutano huo utakuwa wa kwanza unaozikutanisha pande zote mbili tangu ilipoanza operesheni ya kijeshi ya Azerbaijan, ingawa viongozi wa juu wa nchi hizo mbili wamepangiwa kukutana mwezi ujao.
Mkutano wa Brussels utaongozwa na Simon Mordue, ambaye ni mshauri mkuu wa masuala ya kidiplomasia wa rais wa baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel. Ujerumani na Ufaransa pia zitawakilishwa kwenye mkutano huo.