Azerbaijan yamkamata kiongozi wa zamani wa Nagorno Karabakh
27 Septemba 2023Idara ya ulinzi wa mipaka nchini Azerbaijan imesema Ruben Vardanyan, mfanyabiashara tajiri aliyeongoza serikali ya Waarmenia kwenye jimbo la Karabakh tangu Novemba mwaka 2022 hadi Februari mwaka huu amekabidhiwa kwa maafisa wa serikali kuu mjini Baku.
Idara hiyo piaimechapisha picha ya Vardanyan, akisindikizwa na maafisa wawili wa polisi waliobeba bunduki. Taarifa za kukamatwa kwake zimethibitishwa vile vile na mkewe kupitia ukurasa wa mtandao wa Telegram.
Soma pia:Armenia yawapokea zaidi ya wakimbizi 50,000 kutoka Nagorno-Karabakh
Wakati huo huo maelfu ya Waarmenia waliokuwa wakaazi wa jimbo la Karabakh wameendelea kuondoka kwa makundi na kuingia Armenia wakihofia kile wamekutaja kuwa "hatma ya maisha yao"kwenye jimbo hilo lililokuwa chanzo cha mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia kwa zaidi ya miaka 30.