Azerbaijan yapeperusha bendera ya taifa lake Karabakh
15 Oktoba 2023Ofisi ya rais huyo imesema Aliyev, alitoa hotuba na kupeperusha bendera ya nchi yake katika mji ambao Azerbaijan inauita Khankendi na Armenia inauita Stepanakert.
Soma pia:Mahakama ya ICJ, kusikiliza mzozo wa Armenia na Azerbaijan
Eneo hilo la Karabakh ambalo awali lilijulikana kama Nagorno - Karabakh na kwa Waarmenia kama Artsakh, linatambulika kimataifa kama sehemu ya Azerbaijan lakini lilijitenga na kuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya Armenia mnamo mwaka 1994 kufuatia mgogoro uliodumu kwa miaka sita.
Azerbaijan sasa yamiliki eneo zima la Nagorno Karabakh
Vita vilivyofuata mnamo mwaka 2020 vilirejesha sehemu kubwa ya eneo hilo chini ya udhibiti wa Azerbaijan, ambayo shambulio lake kali la mwezi uliopita liliiwezesha kudhibiti eneo lote la Karabakh.