Azerbaijan yatoa waranti wa kukamatwa kiongozi wa Karabakh
1 Oktoba 2023Hiyo ni sehemu ya kampeni yake ya kuwachukulia hatua wale walioongoza mapambano dhidi ya serikali mjini Baku.
Hayo yameelezwa leo mchana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Azerbaijan siku kadhaa tangu maafisa wa nchi hiyo walipomkamata kiongozi mwengine wa vuguvugu la Waarmenia wa jimbo la Karabakh, Ruben Vardanyan.
Vardanyan aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Nagorno Karabakh hadi mwanzoni mwa mwaka huu alitiwa nguvuni siku ya Jumatano akijaribu kukimbia kuelekea Armenia pamoja na makundi mengine ya watu waliolihama jimbo la Karabakh.
Waranti wa kutafutwa kwa Harutyunyan unahusiana na madai kwamba alihusika na mashambulizi ya makombora yaliyoulenga mji wa Azerbaijan wa Ganja, wakati wa vita vya mwaka 2020 vya kuwania jimbo la Nagorno Karabakh kati ya Armenia na Azerbaijan.