AZIMIO LA UCHAGUZI LA VYAMA VYA CDU/CSU
12 Julai 2005Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umeegemea zaidi mauaji ya halaiki ya Srebenica nchini Bosnia na kutangazwa rasmi jana kwa azimio la kugombea uchaguzi ujao la muungano wa upinzani wa CDU/CSU.
Tukianza na gazeti la HANDELSBLATT kutoka Düsseldorf laandika:
“Miaka 10 tangu mauaji ya halaiki ya Srebrenica kizazi kimoja kimepita-kizazi kilichojionea vita magharibi mwa Balkan.Juu ya hivyo, bado dola zinazoregarega na jamii zisizoendelea huko, ndizo zinazogubika sura ya huko.
Uwezekano wa kuporomoka kabisa kwa katiba ya Umoja wa Ulaya na kupungua hamu ya kuwakaribisha wanachama wapya kunaweza kukachangia zaidi kuzuwia kuimarika kwa eneo la magharibi mwa Balkan.”
Nalo gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg linakagua matokeo ya miaka 10 iliopita kwa mema na mabaya yaliotendeka:
Laandika :
“jema ni kuziona nchi za ulaya zimejifunza darasa la kutoweza kufanya kitu kikosi cha kuhifadhi amani cha UM…………….Umoja wa Ulaya unaimarisha misuli yake kijeshi ili kuzuwia msiba kama ule uliozuka (Srebrenica wa kuuwawa kwa waislamu laki 800 wa kibosnia) hautokei tena.Hata Mahkama kuu ya kimataifa mjini The Hague,Uholanzi, imepanda thamani yake.