Upinzani wa Kongo wataka wafuasi kupinga matokeo ya uchaguzi
19 Januari 2024Matangazo
Hata hivyo, Moise Katumbi, Martin Fayulu, na Floribert Anzuluni hawajatoa wito wa kufanyika maandamano. Badala yake wamewasihi wafuasi wao kuelezea kutoridhika kwao, kusimama na kusema hapana kutoka kwenye eneo lolote walipo.
Rais Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa Jumamosi, Januari 20, 2024 mjini Kinshasa kwa muhula wa pili.
Fayulu aliwaambia waandishi wa habari kwamba wamesitisha maandamano ya umma kwa sababu hawawezi kuwapeleka watu wakauwawe. Amesema Wakongomani wote wanajua kuwa uchaguzi huo ulikuwa sawa na mchezo wa kuigiza.
Desemba 27 mwaka uliopita, upinzani uliitisha maandamano, lakini yalipigwa marufuku na mamlaka na kuzuiwa na polisi. Tshisekedi alishinda katika uchaguzi huo wa Desemba 20, kwa asilimia 73.27 ya kura.