Baba yake Marine Le Pen afariki dunia
7 Januari 2025Matangazo
Duru za karibu na mwanawe mwanasiasa huyo mkongwe,Marie Le Pen, zimetoa ripoti juu ya kifo hicho leo Jumanne.
Mwanasiasa Jean Marie Le Pen, aliisaidia kambi ya siasa kali kuzipa mwelekeo mpya siasa za nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka 40 ya harakati zake za kisiasa, akiwavutia wapiga kura wasioridhishwa na sera ya uhamiaji nchini humo pamoja na usalama wa ajira.
Soma pia: Ufaransa: Jean Marie Le Pen afukuzwa kutoka chama chake
Aliwahi kupigania urais mara tano nchini Ufaransa kupitia chama chake cha National Rally ambapo mwaka 2002 aliigia kwenye duru ya pili ya uchaguzi na kushindwa na Jacques Chirac aliyechaguliwa kwa kishindo.