Baerbock na Cameron waisihi Israel ijizuie dhidi ya Iran
18 Aprili 2024Wito huo unatolewa wakati kukiwa na hofu kwamba mvutano wa Iran unaweza kutoka nje ya udhibiti.
Akiwa mjini Tel aviv baada ya kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Rais Isaac Herzog, Baerbock aliisihi kwa mara nyingine Israel kuchukua hatua zake kwa busara na uwajibikaji katika kukabiliana na mashambulizi ya Iran.
Kwa upande wake Waziri Cameron amesema anatumai Jerusalem itajibu kwa njia ambayo ni ya busara, vile vile ngumu na ambayo haitazidisha mzozo huo unaovuta nadhari ya kimataifa.
Soma pia:Israel vitani: Baraza la vita lina jukumu gani katika vita hivyo?
Iran ilifanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Israel siku ya Jumamosi kwa mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora ikujibu shambulio kwenye ubalozi wake mdogo mjini Damascus.
Jumuiya ya kimataifa imetolea wito kwa pande zote kujizuia ili kuepusha mzozo kuwa mkubwa katika eneo hilo la Mashariki ya kati ambalo bado linatafuta suluhu ya vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.