BAGHDAD:Ziara ya ghafula ya Annan nchini Iraq
12 Novemba 2005Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amefanya ziara ya ghafula nchini Iraq.Hii ni ziara yake ya kwanza nchini humo tangu majeshi yaliyoongozwa na Marekani kumpindua Saddam Hussein mwaka 2003.Mjini Baghdad,Annan alikutana na waziri mkuu Ibrahim al Jaafari na viongozi wengine wa kisiasa wa ngazi ya juu.Umoja wa Mataifa umepunguza idadi ya huduma zake nchini Iraq kufuatia mashambulio mawili ya bomu yaliotokea Oktoba mwaka 2003 katika ofisi zake mjini Baghdad.Wakati wa ziara ya Annan,machafuko mapya ya wanamgambo yaliripotiwa na polisi mjini Baghdad.Kwa mujibu wa ripoti ya polisi si chini ya watu 3 wameuawa na wengine 12 wamejeruhiwa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kuripuka karibu ya soko lililojaa watu,kusini mashariki mwa mji mkuu Baghdad.