Balozi wa Ufaransa angalipo Niger licha ya kuamriwa kuondoka
28 Agosti 2023Macron aliyasema hayo katika hotuba yake kuhusiana na sera za nje kwa mabalozi waliokusanyika mjini Paris, ambapo alithibitisha kwamba balozi huyo, Sylvain Itte, bado yuko Niger na alikuwa akifuatilia hotuba hiyo akiwa Niamey.
Soma zaidi: Burkina Faso na Mali zatangaza vita dhidi ya yeyote atakaeivamia Niger
Viongozi wa mapinduzi Niger wasema hawawezi kuupokea ujumbe wa ECOWAS
Macron alisisitiza kwamba Ufaransa isingelibadilisha msimamo wake wa kuyalaani mapinduzi ya kijeshi na kuahidi kumsaidia rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum, akisisitiza kwamba ndiye aliyechaguliwa kidemokrasia na kwamba alikuwa jasiri kwa kukataa kujiuzulu.
Rais Bazoum alipinduliwa Julai 26 na kikosi chake cha walinzi wa kijeshi na tangu hapo amekuwa akizuiwa pamoja na familia yake katika makaazi ya rais.