Lambsdorff: Urusi haina mpango wa mazungumzo ya amani
17 Agosti 2024Balozi Lambsdorff amesema hayo alipozungumza na gazeti la Ujerumani la General-Anzeiger.
Amesema, masharti ambayo Rais Vladimir Putin amekuwa akiyasisitiza kabla ya mazungumzo ambayo ni pamoja na kuitaka Ukraine kuondoka kabisa kwenye maeneo ambayo anaamini wanayadhibiti, yanaashiria kabisa kwamba hana mpango wa kujadiliana.
Amezungumzia pia mafanikio ya mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya Ukraine katika jimbo la Kursk akisema ni wazi yameipa kiwewe Urusi na hasa kwa kuwa yalikuwa ya kushtukiza.
Na alipozungumzia mabadilishano makubwa ya wafungwa kati ya Urusi na mataifa ya magharibi, balozi huyo amesema hayakuashiria kuimarika kwa mawasiliano na Moscow, kwa kuwa Putin hakua na kingine zaidi ya wasiwasi juu ya Krasikov, aliyefungwa Ujerumani baada ya kukutwa na hatia ya mauaji.