Bamako. Uchaguzi kufanyika leo.
29 Aprili 2007Rais Amadou Toumani Toure anatarajiwa kushinda uchaguzi nchini Mali leo, na kuchukua madaraka kwa kipindi cha pili katika uongozi wa nchi hiyo masikini zaidi duniani.
Wapigakura nchini humo wanatarajiwa kwenda katika vituo 20,000 vya kupigia kura na kumchagua mmoja kati ya wagombea wanane wa kiti cha urais katika nchi hiyo iliyokuwa koloni la Ufaransa.
Kampeni zimekuwa zikienda vizuri kwa jumla huku watu wakiimba kauli mbiu za kumsifu rais huyo anayejulikana kwa ufupi ATT ama mpinzani wake mkubwa rais wa bunge la taifa Ibrahim Boubakar Keita.
Toure aliingia madarakani mwaka 1991 kupitia mapinduzi na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kwa kutoa madaraka kwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka mmoja baadaye.