Ban Ki-moon ahimiza wakimbizi kupewa hifadhi
30 Machi 2016Idadi ya wahamiaji waliookolewa katika operesheni zinazoongozwa na walinzi wa pwani ya Italia hadi katika kipindi hiki cha mwaka huu wa 2016 imepanda kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na kipindi kama hiki kwa mwaka uliopita.
Takwimu za wizara ya mambo ya ndani katika kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka huu zinatanabaisha kuwa wahamiaji 16,075, wakiwemo wengine zaidi ya waliowasili salama nchini humo hapo jana, wameokolewa kutoka kwenye maboti ya wasafirishaji haramu ambayo yalikabiliwa na dhoruba katika maeneo ya bahari ya Libya na Sicily. Aidha takwimu hizo zinaonesha katika kipindi kama hiki mwaka uliopita wa 2015, watu 10,150 walifanikiwa kuokolewa.
Operesheni 11 zimefanyika
Walinzi wa pwani wamesema kuwa hapo jana waliendesha operesheni kumi na moja tofatu kwa usaidizi wa meli za jeshi la wana maji la Italia na walinzi wa pwani pamoja na meli za kivita zilizo katika jukumu la operesheni za uokozi za Umoja wa Ulaya. Wahamiaji na waomba hifadhi wanaokolewa wanapelekewa katika bandari za kusini mwa Italia kwa ajili ya kwa ukaguzi wa nyaraka zao.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa yote kuonesha mshikamano na kuwapokea karibu nusu ya wakimbizi milioni moja kutoka Syria hadi ifikapo mwaka 2018.
Wito wa Ban Ki-moon
Akiufungua mkutano wa siku moja wa mawaziri wenye kujadili nanmna ya kuwasaidia zaidi wakimbizi wa Syria na kuhudhuriwa na maafisa zaidi ya 90 kutoka duniani kote, na kuratibiwa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR mjini Geneva Ban alisema utekekezaji wa jambo hilo unahitaji mshikamono wa kimataifa.
Akitolea mfano jitihada za Umoja wa Mataifa zenye lengo la kuumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mitano ambao umesababiosha vifo vya watu 250,000 na wengine karibu milioni 5 kulikimbia taifa hilo wengi ikiwa katika kanda hiyo Ban amesema wapo katika usitishwaji wa uhasama na kwa kiasi kikubwa umetekelezwa kwa zaidi ya mwezi, lakini pande zote zinapaswa kuhimarisha na kutanua jambo hilo katika kusimamisha mapigano na hatimaye kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo.
Takwimu zinaonesha kuwa Uturuki inawahifadhi za wakimbizi milioni 2.7 wa kwa kuanza UNHCR ina lengo la kutenga maeneo ya kuhiwaidhi asilimia 10 kama mwanzo mzuri pamoja na kutotosha. Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anehusika na wakimbizi Filippo Grand, mkapa wakati huu kuna ahadi 179,000 za maeneo mapya ya wakimbizi.
Mwandishi: Sudi Mnetter/ape.
Mhariri: Iddi Ssessanga