Ban Ki-Moon akaribia kuchukuwa nafasi ya Kofi Annan
10 Oktoba 2006Matangazo
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa, wamemteuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya kusini, Ban-Ki Moon, kuchukuwa nafasi ya katibu mkuu wa sasa, Kofi Annan, ambae mhula wake unamalizika. Baada ya kura hiyo, balozi wa Japan kwenye Umoja wa mataifa,Kenzo Oshima, ambae ndiye mwenyekiti wa sasa wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa, alisema wamefanya chaguo zuri. Kwa sasa, wajumbe wote wa nchi 192 wanachama wa Umoja wa mataifa, watapiga kura kuidhinisha kura hiyo ya baraza la usalama kulingana na kanuni za Umoja wa mataifa.