Ban Ki-moon ataka hatua kali dhidi ya Assad
15 Desemba 2011Ban amezungumza mjini New York wakati alipolitumia baraza la usalama la umoja wa mataifa taarifa ya baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu ambayo inasema kuwa zaidi ya watu 5,000, ikiwa ni pamoja na raia na wanajeshi waliokimbia jeshi, wameuwawa tangu Machi mwaka huu. Hadi sasa, Urusi na China zimezuwia juhudi za mataifa ya magharibi kwa baraza hilo kutoa shutuma dhidi ya Syria.
Kundi la wanaharakati wa Syria wanaoangalia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema kuwa raia 21 wamepigwa risasi na kufariki na majeshi ya serikali nchini Syria jana, ikiwa ni pamoja na watu 11 katika mji wa Hama. Vikosi viliingia katika mji huo kuvunja mgomo wa siku tatu kwa ajili ya utu, ulioitishwa na upande wa upinzani. Serikali ya Syria imesema kuwa mzozo huo pia umesababisha wanajeshi 1,100 kuuwawa.