1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki Moon azilaumu nchi tajiri kwa kushindwa kusaidia zile masikini.

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cy0C

DAVOS:

Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa -Ban Ki-moon amezilaumu nchi tajiri duniani kwa kushindwa kuzisaidia nchi maskini na hivyo kuomba kuzidisha juhudi katika vita dhidi ya umaskani.Alikuwa akizungumza katika mkutano wa kiuchumi wa mjini davos Uswisi.Mwana harakati na mwana muziki mashuhuri- bono pamoja na muasisi wa kampuni ya Microsoft-Bill Gates na vilevile mkuu wa umoja wa Mataifa wameweka katika ajenda ya mkutano wa Davos ili yajadiliwe, masula ya kutokomeza ugonjwa wa malarai, kuondoa umaskini pamoja na kubadilika kwa halimya hewa.Mkutano huo umewasomba viongozi wa nchi na mataifa karibu 30 na mawaziri wasiopungu 110.