1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-Moon kuwa kwenye nafasi nzuri kuwa katibu mkuu mpya wa Umoja wa mataifa

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6c

Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya kusini Ban Ki-Moon, amejiweka kwenye nafasi nzuri kuweza kumrithi katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan. Alitoka wa kwanza katika kura ya maoni ya wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa. Balozi wa Uchina kwenye Umoja wa mataifa Wang Guangya alisema kuwa mambo yameanza kubainika:

´´ Kutokana na kazi ya leo, sasa ni wazi kwamba waziri Ban Ki- Moon ndiye mgombea atakayependekezwa na baraza la usalama kwenye mkutano mkuu wa wajumbe wa Umoja wa mataifa´´.

Naye John Bolton kiongozi wa Benki ya dunia, aliongeza kusema kwamba waziri Ban anaaminika vya kutosha:

´´Tunayo heshima kubwa kuwa waziri wa mambo ya kigeni Ban. Tunamjua vizuri kutokana na kazi yake huko Washington na hapa New York. Na tunaamini kuwa ni mtu mashuhuri kikazi na kibinaadamu´´

Baada ya matokeo hayo kutangazwa, hasimu wake mkuu Shashi Tharoor kutoka India, ametangaza kuwa anajiondoa kuwania kiti hicho cha katibu mkuu wa Umoja wa mataifa. Balozi wa Uchina kwenye Umoja wa mataifa Wang Guangya alisema kuwa Baraza la usalama linatarajia kupiga kura kumchagua katibu mkuu mpya wa Umoja wa mataifa ifikapo Oktoba 9 yaani jumatatu wiki ijao. Matokeo ya kura hiyo itabidi yaidhinishwe na wajumbe wa nchi 192 wanachama.