Ban Ki-moon kwenda Pakistan kuwaona wahanga wa mafuriko
14 Agosti 2010Islamabad.
Mtu wa kwanza anayeugua ugonjwa wa kipindupindu ameripotiwa nchini Pakistan kufuatia mafuriko mabaya kuwahi kutokea nchini humo katika miaka kadha. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon , ambaye anatarajiwa kuwasili nchini Pakistan mwishoni mwa juma hili, ameonya kutokea wimbi la pili la vifo kutokana na magonjwa. Ban anatarajiwa kukutana na wahanga pamoja na mashirika ya kutoa misaada. Mkuu wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu Pascal Cuttat amesema.
Mkuu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake John Holmes ametoa wito wa kupatiwa kiasi cha dola milioni 460 za msaada wa dharura. Zaidi ya dola milioni 100 zinahitajika kwa ajili ya kuwahifadhi mamilioni ya watu ambao hawana makaazi. Pakistan na Umoja wa Mataifa zinakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 13 wameathirika na maafa hayo ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,600.