1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-Moon na Dafur

Rainer Suetfeld7 Desemba 2007

Katibu mkuu wa UM ameingiwa na wasi wasi iwapo vikosi vya UM vitaweza kweli Januari ijayo kupelekwa Dafur ,

https://p.dw.com/p/CYef

Katika mzozo wa dafur, nchini Sudan, inakusudiwa kuanza Januari hii ijayo kutumwa vikosi vya pamoja kati ya UM na Umoja wa afrika kuhifadhi huko amani.

Inapangwa kupeleka Dafur kiasi cha askari jeshi 20.000 polisi alfu kadhaa pamoja pia na wasaidizi wa kiraia.

Lakini, wiki 3 kabla mpango huo kuanza ,Katibu-mkuu wa UM Ban Ki- Moon amehadharisha juu ya uwezekano wa kushindwa kutimizwa mradi huo.

Desemba 6,siku 25 kamili kabla halikumalizika jukumu juu ya Dafur la vikosi vya Umoja wa afrika,mpango wenye gharama kubwa kabisa na mkubwa kabisa wa vikosi vya kuhifadhi amani vya UM hauna masharti ya kimsingi kabisa kutekeleza azimio lililopitishwa la vikosi vitakavyochukua nafasi yao.

Na hii ni kinyume na matarajio alioyaeleza hadi sasa Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon:

„Nadhani tuko katika hali ya wasi wasi mkubwa na wakati unapita.“

Alionya katibu mkuu wa UM.

Wanajeshi na polisi 26.000 wa kile kikosi cha „Hybird’ kitakacochangiwa tangu na nchi za kiafrika hata na UM,kilipangwa kupelekwa dafur.Kikosi hiki kiwe na zana bora zaidi kijeshi kuhifadhi amani kuliko lile jeshi la askari 7.000 la Umoja wa afrika liliopo huko wakati huu.

Lakini Ban Ki-moon aonesha kuwa na shaka-shaka kuwa mradi huo utafanikiwa.

„Mkoani dafur tunahitaji uwezo wa kusafiri huku na kule na hasa twahitaji helikopta.lakini hatuna chochote na ndio maana mradi mzima sasa uko hatarini.“

Uwezekano wa kupata zana za usafiri,magari ya vifaru,vyombo vya mawasiliano ya ufundi wa hali ya juu pamoja na utayarifu wa kuingilia popote pale panapozuka fujo katika eneo lenye ukubwa sawa na Ufaransa , ndio ufungo wa kufanikiwa huko Dafur.

Katibu mkuu wa UM akasema kwamba bila ya uwezo barabara wa kusafiri huku na kule hatutakuwa katika hali ya kuweza kuwalinda raia seuze kujilinda binafsi kwa wanajeshi wa UM.

Na haya ndio matatizo yaliochomoza tangu wiki kadhaa kwenye mikutano ya kuchangia vikosi iliofanyika katika Makao makuu ya UM mjini New York.

Uwezekano wa kutuma vikosi hivyo vya UM na UA utapoingia mwaka mpya ,mabingwa wanadai sasa ni ndoto tu.

Hata muda mwengine unaofikiriwa wa majira yajayo ya kiangazi, una shaka shaka.Licha ya bajeti ya matumizi ya kiasi cha dala bilioni 1.4 na licha ya katibu mkuu wa UM kuomba-omba kila pembe ya dunia, hali haitii matumaini kwa wakaazi wa Dafur.

Katibu mkuu alisema na ninamnukulu,

„Nimewasiliana binafsi na kila nchi yenye kuweza kushiriki katika mradi huu.Katika ziara yangu ya Amerika kusin,i nimelizungumzia swali hili kila nilipotembelea.Barani Ulaya na katika ule mkutano wa kilele wa Annapolis,pia nilitoa kilio hicho,bila kuskilizwa.“

Alihuzunika katibu mkuu Ban Ki-moon.

Je, Marekani au Ujerumani zinajificha nyuma nyuma kutoa mchango wao ?

Mchango wa wanajeshi wa nchi za skandinevia na hata China umekataliwa na serikali ya Khartoum.Sudan inataka wanajeshi wasio na zana madhubuti kupelewa Dafur.Hata swali hili ameshindwa Katibu mkuu Ban Kii-monn hadi sasa kulipatia ufumbuzi.Na hii licha ya ahadi za kuridhia alizotoa binafsi rais Al Bashir wa Sudan.Akiungama tatizo lake katibu mkuu alisema,

„Ni kuwa ninakaa kati ya viti vyote bila hata kimoja kukikalia barabara.“

Nchi zanachama wa UM zimesema wazi wazi kile kinachopasa kufanywa huko Dafur,iliobaki ni kutimiza ahadi zao kwa vitendo.