SiasaSudan
Baraza la UN laidhinisha uchunguzi wa uhalifu nchini Sudan
12 Oktoba 2023Matangazo
Katika machafuko ya sasa nchini SUdan, jeshi na kikosi cha Dharura, RSF wamekuwa wakipambana kwa miezi sita iliyopita.
Mataifa 19 yalipiga kura kuunga mkono azimio hilo, 16 yakapinga na 12 hayakupiga kura.
Mwakilishi maalumu wa Marekani kwenye baraza hilo Michele Taylor amesema azimio hilo ni mwito wa kuchukua hatua kwa yale ambayo kila mmoja anakubali kuwa ni masuala muhimu kwa pande zinazopigana ili kuhitimisha ukatili na unyanyasaji mwingine, kusitisha mapigano na kuruhusu upitishjwaji salama wa haraka na usiozuiliwa wa misaada ya kiutu unaohitajika sana.
RSF imekanusha shutuma za watetezi wa haki kuwa iko nyuma yake mashambulizi dhidi ya raia, huku akisema wanajeshi wake watakaopatikana na makosa watafikishwa mahakamani