1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaidhinisha makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza

17 Januari 2025

Baraza la Mawaziri la Usalama la Israel limeidhinisha hii leo makubaliano na Hamas ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4pIWM
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Pool European Pressphoto Agency/AP/dpa/picture alliance

Baraza la Mawaziri la Usalama la Israel limeidhinisha makubaliano na Hamas ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza pamoja na mabadilishano ya mateka, hii ikiwa ni kulingana na ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Uamuzi huo ulitarajiwa licha ya upinzani kutoka kwa baadhi ya mawaziri wa mrengo mkali wa kulia.

Makubaliano hayo sasa yatawasilishwa mbele ya serikali ya muungano ya Netanyahu ili kupewa ishini ya mwisho, itakayofungua njia ya utekelezwaji wake kuanzia siku ya Jumapili.

Makubaliano hayo yatakayotekelezwa kwa awamu tatu, kwanza yatashuhudia kusimamishwa mapigano kwa wiki sita, na awamu ya kwanza pia itahusisha kuachiliwa mateka 33 wanaoshikiliwa na Hamashuko Gaza, lakini pia Israel kuwaachilia mateka inaowazuia kwenye magereza yake.