Barazala la Usalama lataka vita visitishwe Sudan
3 Juni 2023Matangazo
Chombo hicho chenye nguvu zaidi cha Umoja wa Mataifa kimelaani vikali mashambulio ya raia tangu kuzuka kwa mapigano kati ya majenerali wapinzani waliokuwa wakigombea madaraka tangu katikati mwa Aprili.
Soma zaidi:Mkataba wa usitishaji mapigano Sudan warefushwa kwa siku tano zaidi
Aidha baraza hilo limehimiza hatua ya kufikisha haraka huduma za msingi kwa watu wenye uhitaji. Kwa mujibu wa Jumuiya ya Madaktari ya Sudan mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 866 na kuwajeruhi wengine maelfu huku ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.3 wameyakimbia makazi yao.