1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wanusia taji la Bundesliga

11 Machi 2013

Bayern Munich wanashikilia usukani wa Bundesliga wakiwa na pengo la pointi 20 na sasa wamesalia na ushindi wa mechi tatu pekee wakinyakua taji hilo. Wanaweza kutawazwa washindi wa Ujerumani Aprili sita

https://p.dw.com/p/17v4G
Fußball 1. Bundesliga - 25. Spieltag Bayern München - Fortuna Düsseldorf am 09.03.2013 in der Allianz-Arena in München (Bayern). Bayern Münchens Spieler Jerome Boateng (l-r) Bastian Schweinsteiger, Philipp Lahm und Xherdan Shaqiri jubeln nach dem Siegtreffer zum 3:2 durch Boateng. Foto: Luci leonhardt dpa (Achtung, Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z. B. via Bilddatenbanken).) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Bundesliga Bayern München Fortuna DüsseldorfPicha: picture-alliance/dpa

Licha ya kupata pointi moja, kufuatia sare ya bila kufungana na Hanover, Eintracht Frankfurt wameanguka hadi nafasi ya tano baada ya mechi tano mfululizo bila kufunga goli na wakiwa wamefunga tu mabao matano pekee katika mechi zao nane za mwisho kufikia sasa mwaka huu wa 2013. walifunga mara ya mwisho Februari mbili katika ushindi wao wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Hamburger SV. Kufuatia sare hiyo tasa, sasa Hanover wako katika nafasi ya kumi. Hamburg wamesonga hadi nafasi ya sita baada ya kusajili ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya VfB Stuttgart.

Jumamosi, Bayern Munich waliipasha misuli moto tayari kwa mchuano wao wa Jumatano wiki hii wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal, kwa kutoka nyuma na kupata ushindi wa magoli matatu kwa mawili nyumbani dhidi ya Fortnuna Düsseldorf.

Schalke 04 sasa wamewazaba Borussia Dortmund nyumbani na ugenini msimu huu
Schalke 04 sasa wamewazaba Borussia Dortmund nyumbani na ugenini msimu huuPicha: picture-alliance/dpa

Borussia Dortmund ambao wako katika nafasi ya pili, na Bayer Leverkusen katika nafasi ya tatu wote walishindwa. Schalke walijiandaa kwa mchuano wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa kufuzu katika robo fanali nyumbani dhidi ya Galatasaray, kwa kuwashinda majirani zao Dortmund mabao mawili kwa moja. Hata hivyo vijana hao wa samawati watakosa huduma za mchambualiaji wao Klaas-Jan Huntelaar aliyepata jeraha. Schalke ambao waliwashinda pia Dortmund nyumbani kwao mabao mawili kwa moja mwezi Oktoba mwaka jana, sasa wako katika nafasi ya nne baada ya kusajili ushindi wa tatu mfululizo.

Kulikuwa na habari mbaya kwa Dortmund, baada ya beki wa katikati wa Ujerumani Mats Hummels kupatwa na jeraha la tindi ya mguu ambalo litamweka mkekani kwa wiki nne zijazo. Werder Bremen walitoka sare ya goli moja kwa moja na Borussia Moenchengladbach. Greuther Fürth ambao wanashikilia mkia waliduwazwa magoli matatu bila jawabu nyumbani dhidi ya Hoffenheim. Sasa wameweka rekodi mpya ya kuwa timu ya kwanza ya Bundesliga kutoshinda mchuano wowote kati ya mechi zao za kwanza 13 za nyumbani.

Wolfsburg wamesonga hadi nafasi ya 12 baada ya kusajili ushindi wa mabao matano kwa mawili dhidi ya Freiburg ambao wamedondoka hadi nafasi ya saba, wakati Leverkusen wakilazwa goli moja kwa sifuri dhidi ya Mainz ambao wamesonga hadi nafasi ya saba pia.

Champions League

Barcelona itahitaji kufanya kazi ya ziada kuondoa upungufu wa magoli mawili dhidi ya AC Milan kama wangetaka kujiunga na mahasimu wao Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya MABINGWA kesho Jumanne.

Barca sasa watamtegemea Lionel Messi kujaribu kuwaokoa nyumbani Camp Nou dhidi ya AC Milan
Barca sasa watamtegemea Lionel Messi kujaribu kuwaokoa nyumbani Camp Nou dhidi ya AC MilanPicha: picture alliance / dpa

Wakati huo huo mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanapigiwa upatu kujiunga na Borussia Dortmund katika awamu ya timu nane za mwisho. Schalke huenda ikawa timu ya tatu ya Bundesliga kufuzu katika robo fainali kama itaizidi nguvu Galatasaray. Timu nyingine ya Uhispania inayohitajika kutoka nyuma ni Malaga itakapopambana na Porto ambao wanaongoza bao moja kwa sifuri kutokana na mechi ya mkondo wa kwanza.

Arsenal wanakuja Allianz Arena wakiwa na kibarua cha kuyabatilisha magoli matatu kwa moja waliyofungwa nyumbani London. Luiz Gustavo anatarajiwa kuanza katika nafasi ya Bastian Schweinsteiger ambaye yuko nje kutokana na kadi nyingi za njano.

Wakati Premier League ya Uingereza ikionekana kukosa mwakilishi katika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1995/96, Bundesliga huenda ikawa na timu tatu katika awamu hiyo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka wa 1997-98, wakati Bayern, Dortmund na Bayern Leverkusen walipofuzu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA

Mhariri: Mohammed Khelef