1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaionyesha Dortmund nani mfalme wa Der Klassiker

8 Machi 2021

Gumzo la mwishoni mwa wiki lilikuwa ni kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi, kati ya Bayern na Leipzig, na maonyesho ya majogoo wawili wa ufungaji mabao, Robert Lewandowski na Erling Braut Halaand.

https://p.dw.com/p/3qM7A
Bundesliga | Bayern München vs BVB
Picha: Andreas Gebert/REUTERS

Kwanza, Leipzig walihakikisha kuwa wanatuma ujumbe kwa Bayern kuwa hawasalimu amri katika mbio za ubingwa baada ya kuwafunga Freiburg 3 – 0 na kuonja kwa muda mfupi usukani wa ligi, kabla ya Bayern kuwaonyesha watani zao Borussia Dortmund nani ndiye jogoo wa Der Klassiker kwa kuwafunga 4 – 2 katika mechi ya kusisimua uwanjani Allianz Arena. Macho yalikuwa kwa Lewandowski na Halaand. Halaand alianza kwa kufunga mabao mawili ya haraka na kuwalazimu Bayern kutoka nyuma na kushinda huku Lewandowski akipiga hat trick. Huyu hapa kocha wa Bayern Hansi Flick "Hali ya sasa ni kuwa mpinzani akipata fursa, hasa katika dakika za mwanzo, tunaadhibiwa haraka. Lakini naangalia katika upande mzuri, jinsi timu ilivyorudi mchezoni, baada ya 2-0 tukapambana zaidi kimabavu kwa hiyo ikawa muhimu tujionyeshe kuwa tuko tayari kujaribu kurudi mchezoni na tukafanya hivyo kipindi cha kwanza..mwishowe bahati ilichangia pia lakini nadhani tulistahili kwa sababu tulitawala kwa dakika 60 hadi 70 za mchezo.

Mwenzake wa Dortmund alijutia nafasi walizoshindwa kutumia ili kuyalinda mabao yao "Kipindi cha kwanza kilianza vizuri sana na kumalizika vibaya sana. Kuna wakati kulikuwa wa shinikiuo kutoka kwa Bayern. Kuna wakati tulishindwa kufanya mambo 3 - 0. baada ya hapo shinikizo la Bayer likawa kubwa na mambo kuwa 2 -2 kipindi cha mapumziko. tulishindwa kudhibiti shinikizo tena na wakavamia mipira kwenye upande wetu, na mwishowe tukarudi nyumbani mikono mitupu

Dortmund wako nafasi ya sita na pointi 39 nyuma ya Wolfsburg, Frankfurt na Leverkusen

Reuters, AFP, AP