1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yarejea kileleni mwa Bundesliga

24 Septemba 2014

Bayern imerejesha hali ya kawaida katika msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga wakati mabingwa hao watetezi wakiwapiku viongozi wa ligi hiyo Paderborn kwa mabao 4-0 na kuchukua nafasi ya uongozi.

https://p.dw.com/p/1DJbV
Fußball Bundesliga 5. Spieltag FC Bayern München SC Paderborn
Wachezaji wa Bayern Munich wakipongezana baada ya kupata baoPicha: Reuters/Michael Dalder

Munich pia imechupa na kuipita Hoffenheim na Mainz 05, timu ambazo zote zimeridhika na sare na kurejea nyuma kwa pointi mbili nyuma ya Bayern wakati Schalke 04 imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu.

Munich haikusubiri muda mrefu kuweza kupachika bao, ikichukua uongozi katika mchezo huo baada ya dakika nane kwa pasi safi. Arjen Robben alimmegea pasi Thomas Mueller , ambaye aliugonga mpira kwa kisigino na kumfikia Mario Goetze ambaye hakufanya makosa na kuuweka mpra wavuni.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag FC Bayern München SC Paderborn
Mario Goetze akipachika bao dhidi ya PaderbornPicha: picture alliance/augenklick/GES

"Tulikuwa tumejitayarisha sana na mchezo huu. Tulitaka kufanya vizuri kutoka mchezo wetu wa mwisho," amesema Goetze , akimaanisha sare ya bila kufungana kati ya Bayern Munich na Hamburg mwishoni mwa juma lililopita.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag TSG 1899 Hoffenheim SC Freiburg
Hoffenheim wakishangiria bao lililoipa timu hiyo pointi moja dhidi ya FreiburgPicha: picture-alliance/dpa/Uwe Anspach

Wanaoiwinda Bayern wachemsha

Hoffenheim imepoteza nafasi ya kuifuatia Munich lakini Jannik Vestergaard alifunga bao dakika tatu katika muda wa majeruhi na kuiwezesha timu yake kupata sare ya mabao 3-3 nyumbani dhidi ya SC Freiburg na kuifikisha timu hiyo katika pointi tisa.

Jonas Hofmann aliipa Mainz 05 uongozi katika mchezo dhidi ya Eintracht Frankfurt na Shinji Okazaki alipata bao lake la tano msimu huu katika dakika ya 44.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag Eintracht Frankfurt 1. FSV Mainz 05
Wachezaji wa Frankfurt wakishangiria baada ya kurejesha bao dhidi ya MainzPicha: Dennis Grombkowski/Bongarts/Getty Images

Lakini Alexander Maier alipunguza pengo kwa Frankfurt dakika chache kabla ya kuanza dakika za majeruhi kabla ya Seferovic kuweka salama point moja kwa Frankfurt.

Ushindi wa kwanza wa Schalke msimu huu

Schalke imepata pointi zake tatu za kwanza msimu huu baada ya kuikandika Werder Bremen kwa mabao 3-0.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag Werder Bremen FC Schalke 04
Tranquillo Barnetta baada ya kuipatia bao SchalkePicha: Dean Mouhtaropoulos/Bongarts/Getty Images

Tulikuwa na mbinyo mkubwa mno mwanzoni mwa mchezo huu. Lakini tulicheza vizuri katika kipindi cha pili," amesema kocha wa Schalke Jens Keller, ambaye hakuweza kupata huduma ya mchezaji wake wa kati Julian Draxler na Kevin-Prince Boateng ambao wana kadi nyekundu.

Leo (24.09.2014) ligi hiyo inaendelea ambapo Bayer Leverkusen inaweza kuchupa kutoka nafasi ya tano hadi ya pili iwapo itafanikiwa kuikaba koo FC Augsburg inayotembelea mjini Leverkusen.

Borussia Dortmund pia inaingia dimbani leo , ikiwa nyumbani dhidi ya VFB Stuttgart, wakati Borussia Moenchengladbach inaikaribisha Hamburg SV, VFL Wolfburg iko njiani ikiifuata Hertha Berlin na Hannover 96 inaikaribisha FC Kolon.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Mohammec Khelef