1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bazoum yupo salama - jamaa

22 Oktoba 2023

Jamaa wa rais aliyeondolewa madarakani kupitia mapinduzi ya Niger, Mohamed Bazoum, amesema kiongozi huyo yupo na familia yake na anaendelea vizuri.

https://p.dw.com/p/4XsNe
Rais Mohamed Bazoum aliyepinguliwa na jeshi la Niger.
Rais Mohamed Bazoum aliyepinguliwa na jeshi la Niger.Picha: Evelyn Hockstein/Pool/File Photo/REUTERS

Mtu huyo anayehusiana kifamilia na Bazoum ameyasema hayo baada ya madai ya utawala mpya wa kijeshi nchini humo kwamba Bazoum alijaribu kutoroka kifungo cha nyumbani katika ikulu ya rais nchini humo. 

Familia yake imesema daktari wake aliruhusiwa kumuona na kumpelekea chakula.

Soma zaidi: Mawakili wa Bazoum wakanusha madai kwamba alijaribu kutoroka

Siku ya Alhamis, jeshi lililompindua Bazoum lilisema limezuwia jaribio la kiongozi huyo kutoroka. 

Siku ya Ijumaa, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alielezea wasiwasi wake juu ya hali tete iliyopo nchini humo na kutaka Bazoum achiwe huru mara moja pamoja na mkewe na mtoto wake wa kiume.