BEIJING : Taiwan na Korea Kaskazini vyatawala mkutano China
6 Machi 2005Siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Kikomunisti nchini China unaofanyika mjini Beijing masuala juu ya Taiwan na Korea Kaskazini yamehodhi mkutano huo.
Waziri wa mambo ya nje wa China ametupilia mbali wasi wasi wa kuwepo kwa mzozo wa kijeshi na Taiwan.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Li Zhaoxing amesema kwamba muswada wa sheria uliiopendekezwa wa kupiga vita harakati za kutaka kujitenga kwa Taiwan ilikuwa ni kwa ajili tu ya kudhibiti nyendo za Taiwan kuwania uhuru.
Juu ya suala la Korea Kaskazini maafisa wa serikali ya China wanasema njia pekee ya kuutatuwa mzozo wa Korea Kaskazini kumiliki silaha za nuklea ni kuushawishi uongozi wa nchi hiyo kurudi tena kwenye mazungumzo ya mzozo huo yanayozishirikisha nchi sita.