BEIJING:Mjumbe maalum kujadili suala la Myanmar China na India
23 Oktoba 2007Matangazo
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuwasili hapo kesho mjini Beijing China kwa ziara ya siku mbili ya kuwa na mazungumzo na utawala wan chi hiyo juu ya suala la Myanmar.
Mjumbe huyo Ibrahim Gambari amepangiwa ziara ya siku sita katika mataifa ya Asia kwa ajili ya kuzibinya nchi za eneo hilo hususan China na India kuchukua hatua za kuumaliza mzozo nchini Myanmar baada ya kutokea ghasia za hivi karibuni dhidi ya waandamanaji wa kutetea demokrasia nchini humo.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa China Liu Jiangchao Gambari atakutana na mkuu wa baraza la dola Tang Jiaxuan na naibu waziri wa mambo ya nje He Yafei.