1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Mzozo wa biashara ya nguo baina ya China na Marekani waendelea

1 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfS

Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yamevunjika licha ya nchi hizo mbili kufanya mkutano mapema hii leo mjini Beijing.

Wajumbe´wa pande zote mbili Marekani na China wameshindwa kufikia makubaliano juu ya mpango wa wa kupunguza uuzaji wa nguo za China zinazoendelea kutapakaa kwenye masoko ya Marekani.

Marekani imeweka vikwazo vya dharura katika juhudi za kuzuia ungizaji wa nguo nchini humo kutoka China.

Haya yote yanatokea wakati ambapo rais wa China Hu Jintao anatarajiwa kuitembelea Marekani wiki ijayo.