1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Annan amekutana na viongozi wa Lebanon

28 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDHG

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amezungumza na viongozi wa serikali ya Lebanon juu ya suala la kupelekwa vikosi vya kimataifa kulinda amani nchini humo.Hadi wanajeshi 15,000 wa Umoja wa Mataifa wanatazamiwa kupelekwa Lebanon.Kwa maoni ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa,hadi mwishoni mwa juma,kiasi ya wanajeshi 3,500 watapelekwa Lebanon.Kikosi hicho kinatazamiwa kushirikiana na kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 2,000.Waziri wa ulinzi wa Israel Amir Peretz amesema,Israel inataraji kuwa majeshi hayo yatalinda vituo vya mpakani vya Lebanon vile vile.Kiongozi wa Hezbollah,Hassan Nasrallah amehakikisha kuwa wanamgambo wake hawatokuwa na upinzani.Sharti lakini ni kuwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa hawatojaribu kuwanyanganya silaha wanamgambo wa Hezbollah.