1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Israel yashambulia kambi ya wakimbizi wa Ki-Palestina

9 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNC

Vikosi vya Israel vimeshambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina kusini mwa Lebanon.Kwa mujibu wa polisi wa Lebanon,watu 2 wameuawa katika shambulio hilo.Kiasi ya wakimbizi 50,000 huishi katika kambi hiyo karibu na mji wa bandari wa Sidon.Haijulikani ikiwa shambulio hilo lililenga nyumba ya kiongozi mmojawapo wa Hezbollah au nyenzo za Fatah.Mashambulio ya angani ya Israel yameripotiwa vile vile katika eneo la Bekaa kaskazini-mashariki mwa Lebanon.Kwa upande mwingine,wanamgambo wa Hezbollah mara nyingine tena wamerusha makombora kaskazini mwa Israel.Wakati huo huo wanajeshi wa Kiisraeli kwa maelfu wanaelekea kwenye mpaka wa Lebanon. Mapigano mapya ya majeshi ya anga ya Israel yameripotiwa pia katika Ukingo wa Magharibi.Kwa mujibu wa duru za Kipalestina si chini ya watu 2 wameuawa katika mashambulio hayo.