BEIRUT: Mshauri wa Annan akutana na waziri mkuu wa Lebanon
17 Julai 2006Matangazo
Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan kuhusika na masuala ya kisiasa,Vijay Nambiar ameongoza tume iliyokutana na waziri mkuu wa Lebanon,Fouad Siniora mjini Beirut.Nambiar atakaekwenda Israel vile vile, ametoa mwito wa kuachiliwa huru moja kwa moja wanajeshi 2 wa Kiisraeli waliyotekwa nyara na Hezbollah.Hata mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya,Javier Solana amekutana na waziri mkuu wa Lebanon.Mwanadiplomasia huyo wa Umoja wa Ulaya alikwenda Lebanon kwa helikopta ya kijeshi ya Uingereza kutoka kituo cha Cyprus.Solana leo Jumatatu,anangojewa Brussels nchini Ubeligiji kutoa ripoti yake kwa mawaziri wa nje wa nchi za Umoja wa Ulaya.