BELARUS Wanasiasa wawili wa upinzani waadhibiwa
1 Juni 2005Matangazo
Wanasiasa wawili wa upinzani nchini Belarus wamehukumwa miaka miwili ya kazi ngumu kuwarekebisha tabia baada ya kufanya mkutano wa hadhara kumpinga rais Alexander Lukaschenko mwishoni mwa mwaka jana. Mikola Statkevich, kiongozi wa chama cha Social Democratic na Pavel Severinets kiongozi wa chama cha Popular Front, walishtakiwa kwa makosa ya kusababisha fujo.
Belarus imelaumiwa na jamii ya kimataifa kwa kupotea kwa wanasiasa mashuhuri wa upande wa upinzani na ukandamizaji wa vyombo vya habari. Ni taifa la pekee la Ulaya Mashariki ambalo sio mwanachama wa baraza la Ulaya lenye wanachama 46.