Belarus yajiunga na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai
4 Julai 2024Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev alitangaza hatua hiyo na kumpongeza rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko, anayechukuliwa kuwa dikteta wa mwisho wa Ulaya.
Tokayev amesema; Mpendwa Alexander Grigoryevich Lukashenko, katika kipindi kifupi nchi yako imekamilisha taratibu zote muhimu katika kupata uanachama kamili katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Ikiwa hakuna pingamizi, ninapendekeza kuanza mkutano na sherehe ya kutia saini hati za kukubalika kwa Jamhuri ya Belarus kwenye kundi la nchi wanachama wa SCO."
Wakati huo huo, shirika la habari la China CCTV limeripoti kuwa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping ameuambia mkutano wa SCO kwamba wanapaswa kushirikiana kuepusha ushawishi kutoka nje pamoja na kudhibiti mustakabali na hatma ya nchi zao.