1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Dunia yashutumiwa kwa ukiukaji wa haki Tanzania

28 Septemba 2023

Shirika Oakland Institute limeishutumu benki ya Dunia kwa kuifadhili serikali ya Tanzania hivyo kuiwezesha kuendeleza mradi wake unaokiuka haki za binadamu wa kutanua mbuga ya kitaifa ya Ruaha.

https://p.dw.com/p/4WvPS
Rais wa Tanzania Samia Suluhu na Waziri Mkuu wake Kassim Majaliwa
Rais wa Tanzania Samia Suluhu na Waziri Mkuu wake Kassim MajaliwaPicha: Presidential Press Service Tanzania

Kwenye ripoti yake mpya, Oakland Institute limesema Benki kuu ya Dunia imeshindwa kuziwajibisha mamlaka za Tanzania kuhusiana visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji ya kiholela na manyanyaso ya kingono kuhusiana na upanuzi wa mbuga hiyo iliyoko kusini mwa taifa hilo la Afrika mashariki.

Uchunguzi wa shirika hilo uliobaini ushahidi wa makosa ya askari wa mbugani, umesema mradi wa mbuga hiyo kwa kiasi fulani unafadhiliwa na mpango wa Benki ya Dunia wa dola milioni 150 unaojulikana kwa kifupi kama REGROW.

Mnamo Oktoba mwaka 2022, waziri wa Ardhi wa Tanzania alitangaza mpango wa kuwaondoa zaidi ya watu 21,000 kwenye vijiji vitano ikiwemo jamii ya Wamaasai.